Show ya TV ‘In my shoes’ ya mwigizaji
Wema Sepetu kutoka bongo movie imeanza kuonyeshwa Eatv October 16 2013
ambapo Episode hii ya kwanza imeanza kwa kumuonyesha Wema kwanza
akieleza yeye ni nani, anafanya nini, ni mtu wa aina gani na mengine
kama hayo ambapo yafuatayo hapa chini ni maswali aliyoulizwa na
kuyatolea majibu.
Swali: Wema ni nani?
Jibu: Wema Sepetu is a girl, i can say a
Lady mwenye umri wa miaka 24 kutoka familia ya Isack Abraham Sepetu, a
darling, a libra.. a girl who is very ambicious, i love my self…
Swali: Siku yako ya kwanza shuleni ilikuaje?
Wema: Siku ya kwanza tumeenda nikakutana
na msichana flani hivi anaitwa Shubira nakumbuka mpaka leo, alikua
rafiki yangu wa kwanza tulikutana shuleni nilikua na miaka minne…
tumekaa nikaanza kulia kwa sababu ilikua sehemu mpya, mazingira mapya
baada ya hapo tukazoea.
Shule ilikua vipi kipindi unasoma?
Wema: Naweza kusema kipindi ambacho niko
shule, Mwalimu wangu sijawahi kukaa hata siku moja kumfikiria mara
mbili na haijawahi kutokea kwamba hata mwalimu akaweza kufanya labda
matamanio au kutaka kitu chochote, hamna kitu kama hicho
Swali: Utafanya nini ikitokea umerudi shule?
Wema: Ningepata nafasi ya kurudi shule,
academic nini uniform na nini… ningejaribu kuifanya more fun, a place
where everybody can be just himself or herself and just be Wema Sepetu
kwa sababu right now this is my time!!
Swali: Ni nani ambae uko karibu nae kwenye familia yenu?
Wema: Dada yangu wa kwanza kuzaliwa
anaitwa Tunu, tunakwenda sawa kwenye many many ways, kipindi mama yangu
alivyonizaa aliumwa akalazwa hivyo dada yangu ndio akawa ananihudumia
kama mtoto wake, ananinywesha uji… anahakikisha nimekunywa maziwa on
time na mpaka leo ananiita my baby and I call her my mami… mtu wa pili
ni dada yangu wa tatu, she is my bestfriend… baba yangu atabaki kuwa
baba yangu tu, mama yangu ni my gurdian Angel, my heart my darling.
Swali: Ulishawahi kugombana na ndugu zako?
Wema: Yeah nimegombana na dada yangu mpaka sasa hivi hatuongei, sio kitu chepesi….
Swali: Unaamini Mama yako ni mkorofi?
Wema: Linapokuja swala la mama yangu
huwezi ukasema kwamba ni mkorofi lakini hapendi nikikosea wala kufanya
kitu ambacho sicho…. kutokupenda kwake inafikia point anakua na hasira
sana alafu njia ya kuonyesha hasira yake ndio level ya juu, yeye
anafikiria kwamba anatengeneza ila badala ya kutengeneza ndio anaharibu.
Swali: Wema ni mkorofi?
Wema: Mimi sio mkorofi, mtu ambae
hanijui ndio ataniita mkorofi ukishanijua yani tutafika mbali lakini
usiponijua na hujui ninachonitaka ndio tatizo.
Swali: Unajisikiaje kuwa Wema Sepetu?
Wema: Kuwa Wema Sepetu sio kitu rahisi,
haiwezi kuwa kama watu wanavyofikiria na haitakua hivyo kwa sababu ni
maisha ambayo naishi, ni mpaka uone maisha ninayoishi ndio unielewe…
yani hata kujaribu kuieleza ili uielewe napata tabu… mashabiki wangu
wananielewa sana na uhusiano wangu na wao ni mzuri na ni tofauti na
uhusiano kati yangu na familia yangu’
Swali: Unachukulia vipi unaposemwa ama kuandikwa vibaya?
Wema: Katika vitu vyangu ambavyo mtu wa
nje anaweza kuviona kama vile… Mungu wangu Wema ana nini, mi
navichukulia kama changamoto… mi naona kuna kitu special kuhusu mimi,
kwa nini wasiseme watu wengine?
Swali: Unaamini wewe ni mrembo?
Wema: I am beautiful, naamini kwamba mimi ni beautiful kwa sababu nina pure heart… ni kitu Mwenyezi Mungu alichonibariki nacho.
0 comments:
Post a Comment