ABDULKARIM SUMA





Friday, October 18, 2013

Maneno ya Mwinyi Kazimoto kutoka Qatar

Kazimoto-na-gonzalo 
Mwandishi wa stori za michezo Saleh Ally ameandika kwamba kiungo wa Al Markhiya ya Qatar Mtanzania Mwinyi Kazimoto amesema ataendelea kupambana pamoja na ugumu wa ligi hiyo.
Ameonyesha uwezo na kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Al Markhiya inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Qatar ambapo anasisitiza “ligi kweli ni ngumu sana, unajua ushindani unatokana na timu za hapa kuwa na uwezo wa kifedha’

“Wachezaji kutoka Ulaya, Amerika Kusini na hasa Brazil na Argentina wamejazana hapa hivyo kila mmoja anajituma na mimi nimekuwa nikipambana kuhakikisha natoa msaada katika timu yangu’  hiyo ni kauli ya Kazimoto ambae sasa ndie tegemeo namba nane katika kikosi cha timu hiyo.
salehjembe.blogspot.com imeripoti zaidi kwamba kwa mfumo wa Qatar, baadhi ya wachezaji wa ligi kuu wamekuwa wakiruhusiwa kucheza katika mechi za daraja la kwanza hasa kama wanakuwa hawazichezei timu zao za ligi kuu katika timu husika.
Vikosi vya pili vya timu zinazoshiriki ligi kuu viko katika ligi daraja la pili hivyo nyota kadhaa wa ligi kuu wamekuwa wakishuka kwenda kuchezea timu hizo na kuongeza ushindani zaidi.

0 comments:

Post a Comment