Jana tuliweka habari hapa kuwa actress
maarufu Bongo Movies Blandina Chagula(Johari) amekwenda Canada kumfuata
mpenzi wake raia wa nchi hiyo na pia kutambulishwa ukweni. Habari mpya
ni kuwa baada ya kutambulishwa mipango ya ndoa kati ya johari na mzungu
huyo itafanyika ili wawili hao waishi kama mke na mume baada ya mzungu
huyo kuwa hoi bin taabani kwa penzi la Johari aliyejaaliwa kipaji cha
kuigiza. Habari za mipango hiyo ya ndoa zimetolewa na Irene Uwoya
alipozungumza na Bongo5 kwa kusema "akitambulishwa kitakachofuata ni
ndoa, na kwa jinsi tulivyojadiliana watafanya ndoa mbili moja
hapa(Tanzania) na nyingine Canada ili na sisi tulio Dar es salaam
tusherehekee ndoa yake kwasababu kama unavyojua ndugu zake, marafiki na
watanzania kwa ujumla wanahitaji kuhudhuria ndoa hiyo"
Uwoya ambaye nae aliolewa na raia wa Rwanda Hamad Ndikumana kwa ndoa ya gharama na mwishowe ndoa hiyo kuwa chali aliendelea kwa kusema "Juzi niliandika kauli ya kumtaka atulie akiwa Canada, sio kwamba Johari hajatulia unajua Johari ni mtu wangu wa karibu kwa hiyo nilikuwa namwambia asipeleke uswahili Canada sio kwa nia mbaya"

0 comments:
Post a Comment