ABDULKARIM SUMA





Tuesday, November 26, 2013

(News) Mama Lulu ajibu maswali matano muhimu kuhusu Lulu na Kanumba.

1471168_445127252281920_369971201_nALIMKABIDHI LULU KWA KANUMBA?
“Ninachoweza kukiweka wazi ni kwamba, nilikutana na Kanumba nikamkabidhi mwanangu kwa moyo mweupe amlee kisanii kwa sababu nilijua anaweza, kumbe na wao wakaanzisha uhusiano huo kwa siri.

KWA NINI ALIMKABIDHI LULU KWA KANUMBA?
“Mimi na Kanumba tulikuwa tumezoeana sana. Alinipa heshima zote kama mama yake na alikuwa kijana mwenye aibu kwangu kutokana na heshima, haikuwa rahisi kuangaliana machoni na ndiyo maana niliamua kumpa Lulu amkuze kisanii.
ALIPOKEA BARUA YA POSA YA KANUMBA?
“Si kweli, sijawahi kuona wala kupokea barua ya posa ya Kanumba kumchumbia Lulu.
KAMA KANUMBA ANGETAKA KUMUOA LULU?
“Lakini nataka kusema kwamba kama Kanumba angekuwa hai na angetaka kumuoa Lulu ningefurahi sana kwani naamini mpaka sasa wangekuwa wamepata mtoto mzuri na sisi wazazi tukaitwa bibi.”
MADAI YA KUGOMBANA NA MAMA KANUMBA?
Mama Lulu: Mimi na mama Kanumba hatuwezi kugombana hata siku moja. Kwanza Lulu nimempa jukumu kwamba kwa sababu wote ni mama zake, akinunua nyama kilo tano kwa ajili yangu na kwa mama Kanumba apeleke tano.

0 comments:

Post a Comment