Ni
siku kadhaa tu toka baraza la makanisa nchini Kenya (NCCK) kuunga mkono
ombi la viongozi mbalimbali wa Makanisa Mombasa kutaka kumiliki bunduki
aina ya AK 47 ili kujilinda na matukio ya kutisha ikiwemo mashambulizi
dhidi ya viongozi wa Makanisa.
Ni siku kadhaa zimesikika stori za utekwa kwa watu wakiwemo watoto kwenye maeneo mbalimbali ya Kenya.
Kwa kuyaona yote haya, Maseneta wa Kenya wanataka
raia wa nchi hiyo wapewe bunduki kwa sababu hatua hiyo itasaidia
kupunguza visa vya uhalifu huku walikosoa mfumo wa sasa wa utoaji leseni
ya kumiliki bunduki wakisema inawapendelea watu fulani wachache na
kuwabagua Wakenya wengi walioko kwenye hatari ya kushambuliwa na
majambazi wenye silaha.
Walitoa wito kwa Serikali ya Kitaifa kwa wenye umri
wa miaka 30 na zaidi lakini baada kukaguliwa ipasavyo kuhakikisha kuwa
hawawezi kutumia zana hizo vibaya alisema Seneta wa Kajiado Peter
Mositet kupitia hoja aliyowasilisha katika Bunge.
Walikubaliana kuwa wanaotuma maombi wanatakiwa
kufanyiwa ukaguzi wa kina kuhakikisha kuwa wao ni wafanyabiashara,
wafanyakazi wa umma au ni watu wenye mahitaji maalum.
Mositet alisema Wakenya wengi wamehama makwao
kutokana na hofu ya kushambuliwa na majambazi huku biashara nyingi
zikiathirika kutokana na utovu wa usalama katika sehemu mbali mbali za
nchi.
Alisema endapo bunduki zitapewa wanaozihitaji,
asasi za usalama zitakuwa na kazi rahisi kudhibiti usalama na kwamba
ilishuhudiwa wakati wa mkasa wa Westgate pale raia wenye leseni ya kumiliki bunduki walishiriki katika shughuli za uokoaji mali na maisha.
Seneta wa Pokot Magharibi John Lonyangapuo
aliyeunga mkono hoja alisema endapo watu wengi wanapewa leseni za kumili
bunduki majambazi wataogopa kushambulia maeneo ambapo wanajua kuna watu
wanaomiliki.
Mtandao wa Swahili umeripoti kwa kumnukuu seneta
huyo akisema ‘serikali ya Kenya ilikubali kuwa endapo raia wengi
wangekuwa na bunduki, hasara iliyotokana na mkasa wa Westgate ambapo
zaidi ya watu 60 walifariki ingepungua kwa kiasi kikubwa,”
0 comments:
Post a Comment