ABDULKARIM SUMA





Wednesday, December 11, 2013

Baada ya taarifa za kifo chake kwa zaidi ya saa 9, hizi ni picha zake Mzee Small na taarifa kamili.

sm 2
Ni mastaa zaidi ya 10 wa Tanzania ambao wamezushiwa kifo ndani ya mwaka 2013 na stori zote zikawa za uongo baadae, miongoni mwao ni Mwasiti na Mr Blue
….. sasa December 10 2013 kuanzia saa nne usiku taarifa zilezile za kuzushiwa kifo zimemuangukia mwigizaji mzee Small ambae ni kweli kwa kipindi kirefu amekua akiugua.
1. Bado yuko hai ila ana maumivu ya bega na mkono kutokana na mshtuko alioupata toka May 2012.
2. Anasema ‘mlitaka kwenda kuchukua jeneza kutokana na taarifa za kifo cha uongo lakini sasa msichukue, hiyo pesa ya sanda hiyo mchukue mkanunulie watoto chakula wale’
3. Usingizi wao usiku wa kuamkia leo December 11 2013 ulikua wa tabu sana, wamepigiwa simu zaidi ya 10 za watu mbalimbali hata usiku wa manane wakitaka kujua ukweli wa taarifa za kifo.
4. Familia ya Mzee Small inakiri hii ni mara ya pili kwa mwigizaji huyu kuzushiwa kifo ila ya mara hii ndio imekua kubwa kuliko.
5. Mzee Small anasema ‘misaada ya Watanzania kwa njia mbili kaka, kwanza dua zao ndio maana sikufa… mimi sijafa bwana, mimi mzima kabisa, nawashukuru Watanzania ‘
sm 3
sm 4Wakati napiga hii picha, Mzee Small alitania kwa kusema.. ‘Waandishi mmekuja mkijua mtakuta pilau hapa leo sasa hamjaikuta na chai siwapi, mi mzima kabisa tena nawapa dole hili… ‘
sm1Mtu wako wa nguvu nikiwa na familia ya Mzee Small nyumbani kwake Tabata Dar es salaam leo December 11 2013 saa moja asubuhi.

0 comments:

Post a Comment