ABDULKARIM SUMA





Saturday, December 7, 2013

Jacqueline Wolper apatwa na majanga leo siku ya birthday yake. Alma-nusura ajitoe roho



    Leo huku akisherehekea siku yake ya kuzaliwa kwake na huku akiomboleza kifo cha mmoja wa viongozi mashuhuri barani Afrika ndugu Nelson
    mandela aliyetutoka hapo jana, mwanadada Jacqueline wolper amenusufika kuumia kutokana na kupata ajali alipokuwa akisogeza gari lake atoke kwenda kwenye mizunguko yake.

    Jacqueline Wolper alipata ajali ya kugonga ukuta na kuharibu gari lake alipokuwa akitaka kulitoa kwa kile alichosema kuwa ni makosa ya kibinadamu kwani badala ya kukanyaga brake alijikuta akikanyaga pedal ya mafuta kwa bahati mbaya kama alivyofunguka mwenyewe katika ujumbe alioutoa hapo chini

    “…dah kuzaliwa cku moja na kufa ni cku moja nando maana kila cku nasisitiza upendo na chuki zisizokua na sababu.hvii leo ni bthday yangu lakn nilikua nauvaa ukuta wakat nasogeza gar ioshwe tayar kwa maandaliz .wakat nakanyaga brk kumbe nakanyaga mafuta maskn ya mungu nimebomoa matnk ya maji yote nimepasua mabomba yote nimegonga gar nyingne but yote nikumshukuru mungu kwakua sijaumia ila prsh ilishuka kidogo but now npo ok.asante mwenyezi mungu,mungu wa wote,kimbilio la wote na wewe ndo kimbilio langu.niombeeni maskn…”
    Pole sana dada Wolper na Happy birthday kwako.

    0 comments:

    Post a Comment