ABDULKARIM SUMA





Wednesday, December 25, 2013

SHAMSA FORD AGOMA KUOLEWA

STAA wa filamu Bongo ‘Shamsa Ford’ amegoma kuolewa siku chache baada ya tarehe ya harusi yake kufika kwa madai kuwa mambo yalivyopangwa sivyo alivyotarajia.

Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika, zinasema kuwa harusi ya Shamsa ilikuwa ifanyike kati ya Desemba 24 na 25, mwaka huu lakini aligoma kwa vile walikwenda kinyume na makubaliano ya tarehe husika.
“Unajua mwanzoni tarehe ilipangwa nyingine na Shamsa alijiandaa kwa siku hiyo, lakini wanafamilia ya mumewe mtarajiwa wakataka tarehe ibadilishwe ili wafunge siku moja na kaka wa mumewe mtarajiwa yaani shemeji yake ambaye naye pia alikuwa anaoa.
“Ndoa ya shemeji yake ilitakiwa kuharakishwa kwa sababu mchumba wake ana mimba tayari. Kwa hiyo sasa wanafamilia wakaona ni bora kufanya shughuli ya pamoja kwa kuwa wote ni ndugu.. Shamsa akagoma, akataka tarehe ileile waliyokubaliana,” kilieleza chanzo chetu.
Shamsa alipatikana kwenye simu na kufafanua ambapo alisema: “Mimi sikutaka mambo ya kuchanganya harusi mbili kwa wakati mmoja.
Ukizingatia hii ni ndoa yangu ya kwanza halafu leo hii eti tukafanyiwe shughuli pamoja, nitakosa uhuru na sherehe yangu. Mimi nina marafiki wengi ambao wameipania siku hiyo, ndiyo maana niliomba wao waoane kwanza siku hiyo sisi tupange tu mwakani.”

0 comments:

Post a Comment