ABDULKARIM SUMA





Monday, January 27, 2014

PENNY: DIAMOND KAMA CHIZICHIZI VILE!

MTANGAZAJI wa Runinga ya Channel Ten, Penniel Mungilwa ‘Penny’ amefunguka kuwa sifa ya aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ni kama chizichizi lakini kwa undani zaidi ni mtu makini.

Penny alifunguka hayo mbele ya kinasa sauti cha Ijumaa Wikienda hivi karibuni ambapo mbali na kutamka kauli hiyo, alifunguka mambo mengi yaliyohusu penzi lao ambalo alilitaja kuwa wamelipumzisha kwa kupeana nafasi.
Akizungumzia sifa za staa huyo aliyeogelea naye penzini kwa kipindi cha mwaka mmoja na ushee hivi, Penny alisema watu wote wanamjua Diamond ni kama chizichizi vile kutokana na mapepe anayoyafanya akiwa mzigoni lakini linapokuja suala la uhusiano, anakuwa makini sana.
“Diamond ni kama chizichizi vile lakini kwa ndani ni mtu makini sana. Anajua kulea, anajua umuhimu wa mapenzi na anaelewa anatakiwa kumfanyia nini mpenzi wake anapokuwa nyumbani, anajali,” alisema Penny na kuongeza:
Penny.
“Watu wamuanavyo nje na jinsi alivyo katika maisha ya kawaida ni tofauti kabisa, mapepe anayafanya anapokuwa jukwaani na sehemu nyingine zinazohusu kazi yake na si nyumbani.”
Katika aya nyingine, Penny alitiririka na mistari kuwa, baada ya kuona penzi lao limetawaliwa na misukosuko, walikaa chini kwa pamoja na kuamua kupeana nafasi ya kila mmoja wao kufanya mambo yake, hakuna kati yao aliyemtamkia mwenzake kuwa sikutaki.
Alisema katika maisha huwa hapendi vitu vya kuambiwa, hata aliposikia taarifa za Diamond kurudiana na Wema kwa mara ya kwanza nchini China, hakuamini hadi walipokuja kukaa naye na kuzungumza ndipo walipoamua kupeana nafasi.
Diamond.
Hata hivyo, Penny alisema anaamini kuwa Diamond amerudiana na Wema lakini yeye kwa sasa ‘bado yupoyupo sana’, akakiri kuwa anatongozwa na watu tofauti na endapo ikitokea akaamua kuanzisha uhusiano mpya, hatahitaji mtu maarufu kwani anahitaji maisha yake kuwa ya siri, tofauti na zamani.

0 comments:

Post a Comment