ABDULKARIM SUMA





Friday, January 10, 2014

PENNY: THAMANI YA DIAMOND IKO PALEPALE

                                                    Penny akiwa na Diamond enzi za penzi lao.
MTANGAZAJI wa Kituo cha Televisheni cha DTV, Peniel Mungilwa ambaye ni zilipendwa wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnum’ amesema
katika maisha yake haitatokea akamdharau kwa kumkashifu hata kama si wake tena.
Akipiga stori na paparazi wetu, mwanadada huyo alisema japo kwa sasa ametofautiana na Diamond aliyeweka wazi kwamba yupo na Wema Sepetu hawezi kuwa na chuki dhidi yao.
“Naapa kwa Mungu wangu katika maisha yangu haitatokea kamwe nikamdharau Diamond, haijalishi yupo na nani kwa sasa, thamani yake kwangu itabaki palepale hamuwezi jua namheshimu kiasi gani yule mtu,” alisema Penny.

0 comments:

Post a Comment