Inakwenda week sasa toka mkali wa bongo fleva Diamond Platinumz kuonekana kwenye account yake ya Instagram akiwa na ndinga hili kali V8. Mashabiki wakasema mbona lile gari la kwanza alivyolinunua tuliona mbwembwe nyingi za picha na kuliita new baby mara my new toy hili mbona hatuoni hizo mbwembwe? Shabiki mmoja akahoji mbona akipiga picha na hili gari anakaa katikati na kuziba namba za mwanzo zisionekane je ni lake kweli au…?
Na mimi ikanibidi kuzifuatilia picha hizo na kweli nikajionea mwenyewe kama hizo picha zinavyoonekana hapo juu hahaaa…
Sina jibu sahihi mpaka nitakapomtafuta na kutueleza ukweli uko wapi kama ndio new toy au new bby ameingia kwenye himaya ya Platinumz au la… stay tune.
0 comments:
Post a Comment