ABDULKARIM SUMA





Tuesday, January 7, 2014

ZITTO AICHAKAZA CHADEMA SOMA NA ANGALIA PICHA ZA TUKIO ZIMA


 


Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe akiwa ndani ya Mahakama Kuu akisubiri hukumu ya kesi yake leo.

Mwanasheria wa Chadema, Peter Kibatara (kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Sheria na Haki za Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu ndani ya Mahakama Kuu tayari kusikiliza hukumu ya Zitto.
Mwanasheria wa Zitto Kabwe, Albert Msando akiwasili Mahakama Kuu kusikiliza hukumu ya Zitto.
Wanahabari kutoka vyomba mbalimbali wakichukuwa matukio.
Zitto akitoka mahakamani na wapambe wake baada ya kushinda hukumu.
Tundu Lissu akitoka mahakamani baada ya chama chake kushindwa na Zitto.
Albert Msando akiongea na wanahabari baada ya kushinda hukumu hiyo.
Lissu naye akiongea na wanahabari baada ya hukumu.
Ulinzi mkali nje ya Mahakama Kuu.
Lissu akiwatuliza wafuasi wa Chadema.
...Akiongea nao nje ya Mahakama Kuu.
Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo wananchi.
MBUNGE wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Zuberi Kabwe amekigalagaza chama chake baada ya kuibuka mshindi katika hukumu iliyosomwa na Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, John Utamwa.
Hukumu hiyo imetolewa leo majira ya saa 11 jioni baada ya Zitto kuwasilisha shauri la kuiomba mahakama iweke zuio kwa Kamati Kuu ya Chadema (CC) kumjadili kuhusu uanachama wake.
Mahakama Kuu imeamua Zitto aendelee kuwa mwanachama hai wa Chadema mpaka itakamalizika kesi ya awali aliyofungua akidai Chadema kumrejeshea nyazifa zake zote alizovuliwa na chama hicho na kwa kipindi hiki haki zote za mbunge huyo zitakuwa chini ya uangalizi wa mahakama mpaka kesi itakapomalizika na kutolewa hukumu.
Zitto alifungua kesi ya kudai kurejeshewa nyazifa zake ambazo alivuliwa mwishoni mwa mwaka jana, kesi hiyo iliambatana na kesi nyingine aliyoifungua hivi karibuni akiomba Kamati kuu isijadili kuhusu uanachama wake mpaka itakapoisha kesi yake ya awali.
Kesi ya awali yambunge huyo kudai kurejeshewa nyazifa zake itaunguruma tena Februari 13, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment