ABDULKARIM SUMA





Wednesday, February 12, 2014

40 YA MTOTO WA ROSE NDAUKA... MASTAA WASUSA!

UNAFIKI, kubaguana na upendo wa maigizo vimeendelea kuonekana miongoni mwa mastaa wa Bongo baada ya hivi karibuni kususa hafla ya kumtoa nje mtoto wa
mwigizaji machachari, Rose Ndauka aitwaye Naveen.
Tukio hilo lilishuhudiwa na kamera za Risasi Mchanganyiko, lilitokea wikiendi iliyopita, nyumbani kwa msanii huyo, Tandale – Tanesco, Dar, ambapo kichanga chake kilikuwa kimetimiza siku 40 tangu kuzaliwa kwake.
Tofauti na matarajio ya wengi, hafla hiyo ilihudhuriwa na mastaa wachache ambao hata hivyo baadhi yao hawakuonesha ushirikiano wa kutosha – ni kama walikwenda kutembea tu!
Wengi kati ya wachache waliohudhuria walijifungia ndani, wakikwepa macho ya watu badala ya kusaidiana majukumu ya hapa na pale kama ilivyotegemewa.
Wasanii walionekana kuwa bize kumuunga mkono mwenzao ni pamoja na Yvonne Cherry ‘Monalisa’, Suzan Lewis ‘Natasha’, Chuchu Hans na Skaina Ally.
Risasi Mchanganyiko lilimwuliza Rose kuhusu kususwa huko ambapo alijibu: “Siwezi kusema wamenisusia, unajua wakati mwingine huenda wametingwa na majukumu. Nilichokifanya ni kutimiza wajibu wangu wa kuwaalika wenzangu na nilitegemea wangenisapoti.
“Hata hivyo wapo baadhi walitoa udhuru mbalimbali. Nimefurahi kwa waliofika na nimefarijika sana kuja kusherehekea pamoja nami. Nawapenda wote maana ni ndugu zangu.”
Akaongeza: “Pia siwezi kuacha kumshukuru mama yangu mzazi pamoja na mama mzaa chema (mkwewe) kwa kunipa sapoti katika kipindi chote nilichokuwa mjamzito mpaka nilipojifungua salama...  jamani mimba siyo kitu kidogo.”

0 comments:

Post a Comment