ABDULKARIM SUMA





Friday, February 14, 2014

HILI NDILO GARI LILILONUNULIWA NA NAY KWAJILI YA MPENZI WAKE

BAADA ya kumaliza mgogoro wao, msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ anadaiwa kumnunulia gari kali mpenzi wake aitwaye Siwema.

Akistorisha na gazeti hili, Nay alisema aliamua kumnunulia mpenzi wake gari hilo lenye thamani ya shilingi milioni 36 kwa sababu anampenda na alimuahidi kumpa zawadi.
“Siwezi kuficha nampenda sana Siwema ndiyo maana nimempa zawadi ya gari, nilimuahidi nitampa zawadi lakini alikuwa hajui ni zawadi gani, nilipomfanyia ‘sapraizi’ ya gari hilo hakuamini,” alisema Nay wa Mitego.
Hivi karibuni Siwema alitundika picha ya gari hilo lenye rangi ya silva aina ya Toyota Lexus katika ukurasa wake wa Instagram akimshukuru ‘baby’ wake huyo.

0 comments:

Post a Comment