POZI TATA: Ankar katika pozi.
Yeleuuuwi! Siku chache baada ya msanii wa sinema na muziki Bongo,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kujinadi na mchumba wa Kizungu aliyejulikana
kwa jina moja la Ankar, siri imefichuka kwamba jamaa huyo ni mwanaume
tata.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda kutoka London, Uingereza, wikiendi iliyopita, chanzo hicho makini kilisema mwanaume ambaye hivi karibuni Shilole alijinadi kuwa ni bwana’ke siyo kwani huko London baadhi ya watu wanamfahamu kama mwanaume tata kijinsia.
“Yule jamaa anapenda sana kukaa na wanawake, sijawahi kumuona na wanaume wenzake, kazi kukata tu mauno na wanawake. Nilishangaa sana Shilole kusema eti ni mchumba’ke wakati hapa London (Uingereza) ni maarufu sana kwa kushiriki pati za wanawake.
“Maskini Shilole, pale imekula kwake, hakuna chochote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyetishiwa habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Shilole ambapo alikuwa na haya ya kusema:
PIPI YA KIJITI: Ankar akifyonza pipi ya kijiti.
“Jamani imeniuma sana kwani nilikuwa sijui, nimeligundua hilo baada
ya kuambiwa na watu, nilipigiwa simu kutoka Uingereza kwamba yule
mwanaume siyo hivyo sina mpango naye tena kwa kweli,” alisema Shilole
anayetamba na kideo cha Nakomaa na Jiji.
TABASAMU: Ankar akitabasamu katika pozi.
0 comments:
Post a Comment