Mavazi anayovaa msanii wa filamu Elizabeth Michael ‘Lulu,’ sasa yanamuweka matatani kufuatia hivi karibuni kushambuliwa kwa maneno kutokana na kigauni cha kimitego alichokuwa amevaa.
Kigauni hicho ambacho juzikati alionekana nacho mitaa ya Sinza jijini Dar kisha baadaye kukitupia mtandaoni, kimewafanya wengi wahoji anakoelekea msanii huyo anayedai amebadilika.
“Hivi huyu ndiye anayesema amebadilika kweli kwa mavazi haya, mbona anataka kuwapa wakati mgumu wanaume? Ndo ili iweje sasa, ama kweli jasiri haachi asili,” alisema mdau mmoja baada ya kuiona picha hiyo.
Ijumaa lilifanya jitihada za kumtafuta Lulu ili kujua sababu ya kuvaa mavazi hayo lakini simu yake iliita bila kupokelewa.
0 comments:
Post a Comment