ABDULKARIM SUMA





Tuesday, March 4, 2014

Hii stori ya nyama ya Punda kuchinjwa na kuuzwa rasmi Kenya umeipata?

Wakazi wa jiji la Naivasha nchini Kenya bado wanashikilia msimamo wao wa kutoka na imani na ulaji wa nyama ya Punda licha ya mmiliki wa kiwanda cha kuwachinja na kupakia nyama ya
Punda kwa ajili ya soko la Uchina kuthibitisha kwamba amepata soko la kuuza nyama za Punda nchini China.
Mmiliki huyu anasema uwezo wake wa kuzalisha bidhaa hii kutoka kwenye machinjio yake ni peaces 70 mpaka 100 kwa siku, kwa wiki ni mpaka peaces 420.
Baadhi ya Wakazi wa Naivasha wamesema ‘Punda sio ya kuliwa ni ya kufanya kazi lakini wanaifanya kama biashara ya chakula lakini sio chakula, mambo ya kuchinjwa ni mbaya.. mtu auze nyama ile inafaa’
Kwa mujibu wa Standard Media Kenya, hii ni sehemu ya machinjio ya Punda Naivasha.
Kwa mujibu wa Standard Media Kenya, hii ni sehemu ya machinjio ya Punda Naivasha.
Ili kufahamu zaidi kuhusu uchinjaji na uuzaji wa nyama ya Punda nchini Kenya, reporter wa millardayo.com nchini Kenya Julius Kipkoich amezugumza na Afisa mkuu wa afya ya mifugo Wizara ya Kilimo Naivasha.
Afisa huyu aitwae Alex Mathenge anasema ‘Sheria ya Kenya inaruhusu uuzaji wa nyama ya Punda kwa hivyo badala ya watu kujificha wakijaribu kuchinjia hiyo Punda huko msituni ni vizuri wapeleke hiyo Punda kwenye kijiji husika huko Naivasha na hiyo Punda itakaguliwa na kuchinjwa’
Anaendela kwa kusema ‘Baada ya hapo, wale wanaouza nyama hiyo watawaambia Wateja wazi kwamba hii ni nyama ya Punda, kwa hiyo sio vibaya kula nyama ya Punda tena ikiwa imepitia kwenye mazingira sahihi ya kuchinjwa baada ya kupimwa’
Maoni yako ni yapi kuhusu hili mtu wangu? umeshawahi kula nyama tofauti na Bata, mbuzi, kuku au ngo’mbe?

0 comments:

Post a Comment