Hizi ni baadhi ya picha za Fiesta 2013 Dar es salaam ambayo kwa bahati mbata hitilafu ya umeme imesababisha historia kwenye show hii ambayo imekua ikifanyika zaidi ya miaka 10.
Kama shabiki naelewa kabisa jinsi inavyoumiza mzuka kukatizwa kwenye sehemu kama hii ambayo ulikuja kumuona msanii unaempenda, hata mimi kama shabiki nimepata maumivu hayohayo ila yamefanyika maamuzi kwamba show ya Wasanii ambao hawajapanda kwenye stage kama Mohombi, Davido na Diamond itafanyika leo saa tisa alasiri palepale Leaders ambapo hakutakua na kiingilio chochote, hii ni kutokana na kuelewa ni kiasi gani watu wa nguvu watakua wamekwazika kwa kilichotokea mtu wangu, karibu.
0 comments:
Post a Comment