Hayo ni maneno ya mwadada Irene Uwoya aliyoaandika usiku wa leo hii kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii. Tulipoyasoma tuu, tulishtushwa sana kwani si kawaida kwa mwanadada huyu kuandika maneno mzito kama haya na ndipo tulipoamua kufanya utafiti yakinifu ili tujue why??? Na haya ndo majibu ya uchunguzi wetu huu…
Tujikumbushe Historia fupi
Hivi majuzi mwadada Irene Uwoya alipost kwenye mtandao picha za gari yake mpya aina ya Range Rover na ndipo watu wengi walianza ku-comment na “kumponda” mwanadada huyu kuwa sio yake bali kahongwa na wanaume “wanaomuweka mjini”
Irene akajibu
Siku si nyingi baadae Irene aliwajibu kwa kusema kuwa gari hiyo ni yake na wote wanaosema kahongwa watasubiri sana maana hiyo ni matokeo ya jasho lake
Msiba wa baba yake wema wahusishwa
Kwa bahati mbaya mwanadada Wema Sepetu alipata matatizo ya kufiwa na baba yakehivi majuzi na ndipo zikatoka tetesi kuwa ETI mwanadada Irene pamoja na kundi jingine la mastaa Fulani wamesusa kuhudhuria msiba huo kwa madai kuwa Wema huwa hashiriki misiba ya wengine
Mashabiki wa wema wamjia juu
Baada ya mambo hayo yote hapo juu ndipo kundi la mashabiki wa wema walipoanza kuandika kwenye ukurasa wa mwanadada huyo, wakimutukana na kumponda sana eti hilo gari sio lake bali kahongwa na jamaa mmoja hivi (Jina tunalihifadhi kwa sababu za kiusalama) na hivyo asiwadanganye wananchi mambo ambayo si kweli
Uvumilivu ukawa mchache kwa Irene
Baada ya matusi na maneno mengi ya kejeli toka kwa mashabiki hao kumzidi Irene hatimaye ndio ameamua kuandika hayo hapo unayoyaona juu. Daah, hatari sana mjini hapa ukiwa staa.
0 comments:
Post a Comment