ABDULKARIM SUMA





Monday, December 23, 2013

Diamond mwaka huu kavuna thawabu za kutosha huyu hapa tena kwenye sakata la kutoa msaada kwa watoto yatima


1
Diamond amerudi kwao Tandale kwenye kituo cha Al Madina kilichopo Tandale Yemen kuwapa watoto zawadi za Christmas na kupata nao chakula cha mchana.

Wiki iliyopita Diamond alienda kwenye kituo kilichopo Buguruni Malapa na kesho Jumanne ataenda Kigogo kwenye kituo cha New Life.
Baada ya kutoa zawadi za Christmas kule Buguruni alisema kwamba ataendelea kutoa zawadi nyingine kwenye vituo mbalimbali na anawakaribisha watu wengine waungane naye kuwapa watoto zawadi kwenye msimu huu wa sikukuu.
Zawadi hizo zinaambatana na mialiko kwa watoto hao kwenda kwenye show yake maalum kwa ajili ya watoto itakayofanyika siku ya Christmas pale Leaders Club.
Hizi hapa ni picha jinsi mambo yalivyokuwa huko Tandale Al Madina.
2
3
4
5
6
7
8

0 comments:

Post a Comment