ABDULKARIM SUMA





Sunday, January 12, 2014

ARIEL SHARON AFARIKI



Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon enzi za uhai wake.
Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon amefariki dunia leo Januari 11, 2014.
Sharon, aliyekuwa Waziri Mkuu wa 11 wa taifa hilo la kiyahudi, alikuwa kiongozi wa chama cha Likud, lakini katika mzozo mkubwa ndani ya chama hicho kufuatia tofauti za kimtizamo kuhusu ukanda wa Gaza, alijitoa Novemba 2005 na kuanzisha chama chake cha Kadima akiwa bado madarakani.
Alitegemewa kushinda katika uchaguzi uliotarajiwa kufanyika baadaye, lakini ghafla Januari 4 mwaka 2006 alipata ugonjwa wa kupooza mwili mzima na alibakia katika hali hiyo mbaya kwa muda wa miaka nane hadi alipofariki leo.

0 comments:

Post a Comment