Ikiwa ni siku ya tatu tangu kuachiwa kwa video ya Rapa toka kundi la Tip Top Connection Madee video ya wimbo wa wimbo wake wa Tema Mate Tuwachape baadhi ya maoni ya
watu yamekua ni shaka juu ya video hiyo na kusema kuwa ya kawaida kulingana na ilivyotegemewa kwa yeye kwenda kufanyia nje ya nchi.
Millardayo.com kama kawaida yake ilimtafuta Madee na kumuuliza juu ya hili suala,Madee anaanza kwa kusema>>‘Unajua huwezi kupata wote wanaosifia na huwez kupata wote ambao wanachukia na kwenye vitabu vyetu vya Quraan vinasema hauwezi ukapendwa na watu wote’
‘Ukipendwa na watu wote wewe una kasoro na ukichukiwa na watu wote pia una kasoro kwa hiyo unatakiwa kubalance Kuna watu wengine wananambia kitu Fulani na kitu Fulani hujakipatia umefata nini Kenya hao wapo na kuna wengine wanasema yes mwanangu saivi kweli unaonyesha jinsi gani umebadilika kama nyimbo yenyewe inavyosema,hivyo ni changamoto nafurahia kuona watu wameangalia na kila mtu kasema chake’.
Hii ni video ya kwanza kwa Rapa Madee kwenda kufanya na Ogopa Video ya Kenya,waweza kuitazama hapahapa Millardayo.com,tumia sekunde kadhaa kumsikiliza madee akielezea maoni ya watu alivyoyapokea.
Bonyeza play kusikiliza.
0 comments:
Post a Comment