STAA wa sinema Bongo, Aunt Ezekiel amejikuta akizichapa na mwanamke aitwaye Sarah Mwakapala ambaye miaka mitano iliyopita waliwahi
kugombea penzi la mwanaume anayejulikana kwa jina la Mwilu Mwilola ‘Silva’.
Tukio la ugomvi huo lilichukuwa nafasi juzi katika Ukumbi wa Letasi Lounge uliopo Victoria jijini Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ya rafiki yao aliyetambulika kwa jina la Jamila.
Ilielezwa kuwa, wakati sherehe ikiendelea, Sarah alisimama na kwenda mahali alipokaa Aunt na kuanza kumfanyia fujo huku wageni waalikwa wakishind
wa kujua chanzo.Chanzo kilichoshuhudia sekeseke hilo kilibainisha kuwa, Aunt alionekana kujishusha akimwomba Sarah kuacha mambo ya ugomvi, lakini Sarah hakukubali ndipo mtiti ulipozidi kuwa mkubwa na kusababisha wavuane mawigi yao yaliyokuwa yamewapendeza.
“Ghafla tulishangaa Sarah anainuka na kwenda kumvamia mwenzake pasipo kujua nini chanzo. Sijui wenyewe bado wana mabifu yale ya kipindi kile au vipi!” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, mdau maarufu wa mastaa wa Kibongo, Nice Chande ambaye alikuwa karibu na Aunt, aliingilia ugomvi huo na kutuliza hali ya hewa kwa kumdhibiti Sarah.
“Unajua kuna watu hawajifunzi kwa wenzao kuhusiana na vifo vya siku hizi, we unakuja kumfanyia fujo mwenzako, mnapigana bila sababu yoyote. Je, ghafla mwenzio siku zake za kuishi kumbe zimeisha unapata kesi la ajabu, unaanza kujilaumu,” alisema Nice.
Baada ya hali ya hewa kutulia, paparazi wetu alimfuata Sarah kutaka kujua kulikoni amuanzishie fujo mwenzake, hakuweza kujibu chochote huku akiingia kwenye gari na kukimbilia Kituo cha Polisi Oysterbay kufungua kesi.
Taarifa zilizopatikana baadaye wakati gazeti hili linakwenda mitamboni zinadai kuwa, Aunt naye alikimbilia polisi na kukuta Sarah ameshafungua malalamiko lakini waliyamaliza palepale kituoni na msala ukaishia hapo.
0 comments:
Post a Comment