ABDULKARIM SUMA





Thursday, January 16, 2014

FEROOZ MBARONI KWA BANGI

Mwanamuziki Ferooz Mrisho akiwa mikononi mwa polisi baada ya kunaswa akivuta bangi.
NYOTA aliyetamba katika muziki wa kizazi kipya enzi hizo akiwa na Kundi la
Daz Nundaz, Ferooz Mrisho, juzikati alikamatwa na polisi na kutupwa lupango katika Kituo Kidogo cha Mabatini, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, baada ya kukutwa akivuta bangi pamoja na vijana wenzake kadhaa maeneo ya Sinza, karibu na Baa ya Meeda.
Habari zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda na baadaye kuthibitishwa na gazeti hili, zilisema Ferooz alikuwa akivuta bangi katika eneo hilo kabla ya majirani wanaokerwa na tabia hiyo, kupiga simu polisi wakitaka kukomeshwa kwa jambo hilo.
“Hapana tumechoka na tabia zao, kila ukipita hapa unakula ‘marashi’ ya bangi tu, vilevile sisi tuna vijana wa rika lao, hawa vijana wanaopita hapa wanasoma,  tunaogopa sana wasije wakajiunga na wao hapa kula ganja,” alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Ferooz akiwa amepigwa pingu na mwenzake.
Ilidaiwa kuwa msanii huyo pamoja na wenzake wamekuwa na kawaida ya kukaa katika kijiwe hicho kila siku na kuvuta bangi huku baadhi yao wakitumia madawa ya kulevya.
Baada ya kutiwa nguvuni kwa vijana hao, wakazi wa maeneo hayo wamewamwagia sifa Mkuu wa Kituo cha Polisi Mabatini aliyefahamika kwa jina moja la Mapunda kwa jinsi alivyofanikisha askari kuwahi eneo hilo la tukio.
...Akishushwa kutoka kwenye gari.
“Tulipopiga simu polisi, hatukutegemea kama ingekuwa haraka hivyo, tunashangaa baada ya muda mfupi, wakaja eneo hili, kwa kweli huyu mkuu ni mfano wa kuigwa, maana siku hizi likitokea tukio lolote lile ni dakika chache gari limefika,” alisema mkazi mmoja wa eneo hilo.
Ferooz, mkali wa kibao cha Starehe baada ya kufikishwa kituoni hapo alichukuliwa maelezo yake kabla ya kuwekwa rumande. Hadi gazeti hili likienda mitamboni haikufahamika siku ya kufikishwa mahakamani kwa wahalifu hao.

0 comments:

Post a Comment