Mwezi December 2013 taarifa zilitoka kwamba kuna binti wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 aliekamatwa na dawa za kulevya huko Macao China
ambapo baadhi ya taarifa zilizoripotiwa na Waandishi wa Tanzania zilisema aliekamatwa ni mrembo ambae amekua akionekana kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva (Jackie Cliff).
Ubalozi wa Tanzania nchini China umezungumza kwenye Exclusive interview na millardayo.com na kusema yafuatayo >>> ‘Uongozi wa hapa haujatujulisha chochote wala kutuandikia, kwa taratibu zetu sisi kama balozi watu wote ambao wanakamatwa hapa kwa makosa ya aina yoyote ile serikali husika zinatuandikia, zikituandikia zinasema alikamatwaje na walichukua/watachukua hatua zipi, na kama wameshamfungulia mashitaka wanatujulisha, mpaka sasa hatuna taarifa yoyote kutoka kwa Serikali kuhusu hilo la Jackie’
millardayo.com : Mara ya mwisho kupata taarifa za Mtanzania kukamatwa na dawa za kulevya China ilikua lini?
Balozi: ‘Ninazo taarifa nyingi ila ni kama mwezi uliopita alikamatwa Mwanaume, ni Wanaume waliokamatiwa Guangzhou, mtu wangu aliekua anafatilia pia amekuja leo January 9 2014 asubuhi na kuniambia hakuna taarifa zozote kuhusu Jackline Patrick Cliff’
Kama ni Macao wangetuandikia moja kwa moja, Macao na Hongkong wangetuandikia moja kwa moja na kama wangekua wamewasiliana na balozi wetu wa heshima kule Hongkong pia wangetuandikia, Wachina mtu yeyote wanaemkamata ambae anatumia hati ya kusafiria ya Tanzania wanamuhusisha kama raia wa Tanzania kwa hiyo wanajulisha ubalozi wake labda mtu mwenyewe aseme ni wa taifa jingine, watatuandikia hivyohivyo nakueleza…..’
*************************
Baada ya hayo maelezo ya Ubalozi wa Tanzania huko China, maswali yanabaki…. Jackie Cliff yukwapi? mbona marafiki wanasema hawampati kwenye simu? na huyu Mtanzania binti wa miaka 28 aliekamatwa Macao ni nani?
kaa karibu na Millard Ayo kwenye facebook, twitter na instagram na millardayo.com yenyewe manake stori bado inafatiliwa, ukishajiunga kuwa Mwanafamilia ni uhakika kwamba chochote kikitokea utajulishwa hata kama ni usiku wa manane.
0 comments:
Post a Comment