MWANAMITINDO Jacqueline Patrick ambaye yuko nyuma ya nondo, Macau nchini China kwa madai ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya heroine, amesherehekea siku yake ya kuzaliwa (Januari 13) mwaka huu akiwa gerezani.
Mpenzi wake wa sasa Juma Khalid ’Jux’, amemwandikia ujumbe mzito mpenzi wake huyo kupitia Mtandao wa Kijamii wa Instagram na kueleza hisia zake.
“Kwa kweli nilizoea sana kuongea nawe siku kama hii ya kuzaliwa kwako na umekuwa mtu muhimu sana kwangu, siwezi kueleza... tabasamu lako siku zote limenifanya niwe na furaha,“ aliandika Jux.
Baada ya Jux kuandika ujumbe huo wadau mbalimbali walionekana kumpongeza kwa kuikumbuka siku hiyo ya mpenzi wake ingawaje hivi sasa yupo matatizoni.
Juma Khalid ’Jux’ akiwa na mpenzi wake Jack kabla hajakamatwa.
Mwandishi wetu alimpigia Jux na kumwuliza zaidi kuhusiana na ujumbe
wake huo ambapo alisema: “Siwezi kuzuia hisia zangu kwa Jack, ingekuwa
siku yenye maana sana kwangu na kwake kama ningekuwa naye lakini ndiyo
hivyo tena mwenzangu yupo kwenye matatizo.”
0 comments:
Post a Comment