LORI la mafuta ambalo namba za usajili hazijatambuliwa wala kampuni inayolimiki, limepinduka mchana huu maeneo ya Kimara-Stop Over jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo, kondakta ameokolewa isipokuwa dereva ambaye inasadikiwa amekufa bado mwili wake umekandamizwa na lori hilo, polisi kwa kushirikiana na wananchi wanafanya jitihada za kumtoa.
Shuhuda huyo amesema vijana ‘wahuni’ wa maeneo hayo, badala ya kusaidia kuokoa wanaiba mafuta kwa kutumia ndoo na kwamba eneo hilo limetawaliwa na fujo na msongamano mkubwa wa magari na watu.
0 comments:
Post a Comment