Wenyeviti wa CCM mikoa ya Tanzania bara wametoa tamko la kumkana Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti CCM Taifa Mgana Mzindakayi la kutowauza wenyeviti wenzake kwa watu wanaotarajia kugombea urais kabla ya muda na utaratibu wa Chama kufika.
Hatua hiyo inafuatia tamko lililotolewa kwa niaba ya Wenyeviti wa CCM wa mikoa ya Tanzania bara Joseph Msukuma leo jijini Mwanza kufuatia kauli iliyotolewa hivi karibuni na Msindayii ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida alipoalikwa kwenye sherehe ya kuuaga na kuukaribisha mwaka mpya wilayani Monduli
Kwenye hafla hiyo iliyoandaliwa na Mjumbe wa NEC na mbunge wa Monduli Mhe. Edward Lowassa ambapo katika salamu zake Msindayi alinukuliwa na vyombo vya habari na taarifa zake kutoka leo akisema kuwa yeye pamoja na wenyeviti wa CCM wa mikoa yote nchini wako nyuma ya Lowassa wakimuunga mkono kauli ambayo imewaweka katika wakati mgumu na wenyeviti wa CCM mikoa mbalimbali hapa nchini kwa kuanza kuwagawa na kutengeneza makundi.
hiki ndicho walichokisema wenyeviti Ccm Tanzania Bara 2014
0 comments:
Post a Comment