ABDULKARIM SUMA





Friday, February 14, 2014

ALHA: MAPEDESHEE NI JANGA SIJUI NINI KIMEMKUTA MISS TZ STORY HAPA


MISS Tanzania 2011, Salha Israel ametoboa siri kuhusiana na mapedeshee ambao wamekuwa wakiwapa usumbufu mkubwa kiasi cha kuonekana ni janga la kitaifa kwa
warembo.
Miss Tanzania 2011, Salha Israel.
Akizungumza na Ijumaa kwenye mahojiano maalum hivi karibuni ndani ya ofisi za gazeti hili, Salha alikiri kuwepo kwa watu wenye nia mbaya wanaotumia utajiri wao kujipatia wasichana hali inayosababisha kuichafua Miss Tz.
“Kusema ukweli nilipokuwa kwenye shindano hili sikupata usumbufu sana ila baada ya kupata taji, usumbufu ukaanzia hapo.
“Nikawa napigiwa simu na watu nisiowajua huku wengine wakitaka nionane nao, nimekuwa nikiwakwepa ila ni wasumbufu mno,” alisema Salha aliyekuwa ameongozana na wadogo zake Sabra na Samier.

0 comments:

Post a Comment