ABDULKARIM SUMA





Friday, February 14, 2014

ANTI LULU ANASWA NA NJEMBA

MWANADADA asiyeishiwa na matukio Bongo, Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ juzikati alinaswa ‘live’ akiwa kimalovee na mcheza soka wa zamani aitwaye
Amani Simba.
Wawili hao walibambwa kwenye ufukwe wa Coco, Oysterbay jijini Dar wakipunga upepo na walipowaona mapaparazi wa gazeti hili walishituka na kutaka kujificha.
Akizungumzia uhusiano wake na Amani, Anti Lulu alisema: ”Jamani acheni udaku wenu, siku hizi nimetulia na huyu ndiye mchumba wangu, nampenda sana na yeye hivyohivyo.”
Hata hivyo, chanzo makini kilicho karibu na wawili hao kimedai kwamba kwa sasa wanaishi pamoja.

0 comments:

Post a Comment