
Imepita miezi kadhaa toka aachie wimbo wake wa Nimevurugwa ambapo kuhusu video ya wimbo huo kuna taarifa kuwa mamlaka husika imeifungia hiyo video,leo kupitia millardayo.com Snura katubariki kutupatia wimbo huu ambao rasmi anauachia mwishoni mwa February.
Kwa maelezo ya haraka haraka kuhusu wimbo huu Snura kaongela watu wenye kuiangalia leo na sio kesho kwa mfano mtu anaamua kuuza nyumba kwa kupunguza matatizo ya leo na hatima yake kesho anakosa pa kulala.
Nafasi nayokupatia mtu wangu wa nguvu ni kusikiliza kipande hiki kidogo cha huu wimbo wakati tukisubiri Mwisho wa February akiruhusu kukupatia wimbo wote ukiwa kamili.
Bonyeza play kusikiliza.
0 comments:
Post a Comment