Mambo matano Yatakayokugusa katika maisha ya Diamond Platnumz
01. Diamond Platnumz aliachwa na baba yake
Diamond
alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es
salaam. Akiwa na umri mdogo wazazi wake walitengana na baba yake
kumuacha bila msaada wowote. Hapa chini huyo ndiyo baba yake diamond.
02. Chumba kupangishwa ili kumsomesha
Baada ya
wazazi wake kutengana, Diamond aliamia kwa bibi yake huko tandale na
ilipofika muda wa yeye kwenda sekondari ilibidi bibi yake apangishe
chumba kimoja ili Diamond aende shule na ikabidi alale chumba kimoja na
bibi na mama yake.
03. Aliacha shule kwa kukosa Ada
Diamond alikua na akili darasani na
alipomaliza elimu yake ya O’level ilikosekana pesa ya kumpeleka A’level na hapo ndio ilikua mwisho wa elimu yake.
04. Diamond ameshafanya kazi viwandani, Kafanya kazi za kupigisha simu , kuuza mitumba na kuuza maji.
Kuna
kipindi Diamond alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi
kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8.
05. Mama yake alisaidia sana kutoka kwake
Mama yake
alikuwa anampeleka kwenye talent show na kumsubiria hadi usiku mpaka
aperform ndo wanarudi wote. Ndugu zake wengine waliona anamdekeza
mwanae.
0 comments:
Post a Comment