Kauli ya Wema imekuja siku chache baada ya Jokate
kufika kwa kushtukiza katika onyesho lililofanywa na Wema mkoani Arusha hivi karibuni na kumaliza tofauti zao.
Wawili hao wanadaiwa walikuwa wakimgombea mwanamuziki nyota na tajiri, Diamond Platinum.
“Sikuona kioja wala ajabu, kwa kuwa tulikuwa marafiki na kilichotokea ni ujana. Kila mmoja amekaa na kuona hakuna haja ya kuwa na bifu zisizokuwa na faida. Nimemuunga mkono Jokate kwa kuwa ameonyesha kukua na kukomaa kiuamuzi, hakuna haja ya kumbeza kwa maneno ya kijinga,”alisema Wema.
0 comments:
Post a Comment