Ligi kuu ya England imeendelea hii leo kwa kushuhudia ratiba ya ligi hiyo ikiwa na mechi saba zinazokutanisha timu kumi nane kwenye viwanja tofauti.
Jijini Manchester mchezo wa kwanza uliowakutanisha vinara wa ligi hiyo Arsenal Manchester City uliisha kwa ushindi kwa Manchester City ambao waliwafunga washika bunduki wa jiji la London kwa mabao sita kwa matatu .
Katika mchezo huo City walifunga kupitia kwa Fernandinho aliyefunga mabao mawili , Sergio Aguerro , Alvaro Negredo na Yaya Toure huku Arsenal wakifunga kupitia kwa Theo Walcott ambaye alifunga mabao mawili na beki Per Mertersecker.
Matokeo haya yanamaanisha kuwa Manchester City wameikaribia Arsenal ambapo tofauti ya pointi baina ya timu hizo ni pointi tatu pekee ambapo Arsenal wanaongoza wakiwa na pointi 35 huku City wakiwafuatia kwa pointi 32.
0 comments:
Post a Comment