Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere huenda akaingia matatani baada ya kuwaonyesha mashabiki wa Man City ishara ya matusi kwa kidole chake sekunde chache baada ya mchezo ambao Arsenal ilifungwa 6-3 kumalizika
.
Wilshere akiwa anaonekana kukerwa na kelele za mashabiki hao ambao walionekana kuimba nyimbo za kumdhihaki aliwaonyesha kidole cha kati ishara ambayo hutafsiriwa kama tusi sehemu mbalimbali duniani.
Kutokana na kitendo hicho Wilshere yuko hatarini kukumbwa na rungu la chama cha soka cha England FA ambao kwa vyovyote watalifanyia uchunguzi tukio hilo kabla ya kulifanyia maamuzi.
Mara nyingi wachezaji wanaofanya kosa kama hilo hukumbana na hatua za kinidhamu ikiwemo kutozwa faini pamoja na kupewa adhabu ya kufungiwa mechi kati ya mbili na tatu.
Hii itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo kuingia matatani baada ya kupigwa picha akiwa anavuta sigara ndani ya klabu ya usiku huko London wiki chache zilizopita .
Wachezaji kadhaa akiwamo David Beckham na Luis Suarez wamewahi kukumbana na adhabu tofauti baada ya kufanya kosa kama hilo.
0 comments:
Post a Comment