‘Abiria wote walipoteremka dakika 3 yule jamaa akarudi tena ndani ya basi utaratibu wangu watu wote wakishuka huwa nafunga milango ya gari kwa rimoti mpaka watu wote wakimaliza kula tunaingia tena ndani ya basi kwa pamoja kwa ajili ya usalama zaidi’
‘Jamaa alivyopanda nikashangaa huyu jamaa mbona amepanda kabla ya watu kumaliza chakula nilivyoenda kumuangalia nikamkuta ana sime yuko kwenye boneti yani eneo langu la kazi yaani nikiwa na maana sehemu ya kitanda nikamkuta anajichoma kisu aina ya sime’
‘Nikaanza kupiga kelele watu wakajaa tukamuita Meneja wa hotel akapiga simu polisi baada ya nusu saa wakaja polisi lakini walikuta jamaa yuko hoi ameshalala chini na damu zimetapakaa kwenye gari’
‘Yule jamaa nilipata neno lake moja anaitwa Kulwa kwa sababu yule ndugu yake alivyokuja akaanza kupiga kelele huku akiita ‘Kulwa kwanini unajiua,kulwa kwanini unajiua’baada ya hivyo yule ndugu yake akaanza kukimbia’
‘Tulimfukuza akarudi pale akaanza kusema kuwa huyu jamaa alikuwa anafanya kazi Lindi hakuwa na cha kuzungumza pale,baada ya polisi kuja wakamchukua jamaa wakamuweka chini ya ulinzi na Yule jamaa mwingine tayari macho alikua kashaanza kugeuza geuza’
‘Sisi tuliendelea kusubiri kuanzia hiyo saa 9 Alasiri mpaka saa 11 jioni mkuu wa kituo wa Kilwa Masoko alivyokuja kunihoji,mwisho wa mchezo Yule jamaa akapelekwa Kilwa Masoko,lakini siku ya pili wakati tunarudi Mtwara tulipishana nae na gari ya polisi analetwa Muhimbili baada ya Madaktari wa Kilwa Masoko kushindwa hilo zoezi’
‘Pale hakufariki watu wote tuliamini amefariki maana macho alishafumba na alikua hana uwezo maana hatua ya mwisho wakati anataka kudondoka chini aliomba karatasi na kuandika ‘kaka’ halafu akakata kauli hakuweza kuandika tena lakini aliashiria tumkamate yule jamaa yake aliesafiri nae alikua akiashiria kwa mikono yake’
‘Humu ndani tulipakia wamasai 3 wale wamasai nahisi walivyoteremka pale Nangulukuru kula mmojawapo alikua na Sime ambayo aliiacha kwenye kiti,walikua wamekaa siti namba 6 na 9 ni karibu na mbele hapa,nafikiri walipoteremka jamaa aliliona lile sime na ndiyo maana wao walivyoteremka tu kwenda kwenye chakula yeye akarudi kwenye basi’
‘Nafikiri alilidhamiria lile sime ndiyo maana alivyoingia tu alifanya kile kitendo bila kuchelewa na wale wamasai baada ya kuja polisi wakakataa lakini wawili walikua na mapanga yao kiunoni lakini yule mmoja akakataa akasema ameliacha pale alisafiri na rungu tu’.
Tunaendelea kufatilia kujua hali ya mgonjwa ambapo jeshi la Polisi Lindi tayari limethibitisha kwamba abiria huyu hakupoteza maisha kama wengi walivyodhani, endelea kuwa mwanafamilia wa millardayo.com kwa kujiunga na mimi kwa jina hilohilo la millardayo kwenye facebook instagram na twitter ili uendelee kupata habari za uhakika usiku na mchana.
0 comments:
Post a Comment