Kampuni
ya Proin Promortion ambayo in ashughulika na uongozaji na usambazaji wa
filamu mbalimbali za Kitanzania February 20 wamezindua Filamu mpya 3
ambazo zinategemewa kuingia sokoni hivi karibuni.
Movie
hizo ni pamoja na Network,Mdundiko na Sunshine ambayo ndani yake yupo
mkali wa Rnb Ben Pol,Movie hizi zimezinduliwa pale Century Cinemax
Oysterbay ambapo baada ya kuzinduliwa kila mmoja alipata nafasi ya
kuchagua movie aliyotaka kuangalia.
Upande
wa waongozaji filamu hizi zimeongozwa na waongozaji[Directors]watatu
ambao ni John Kalaghe,Karabani na Jackson Kabiligi kwa Jackson hii ni
filamu yake ya kwanza kuiongoza na miongoni mwa Mastar walihudhuria ni
pamoja na Dr.Cheni,Jb,Check budi,Marlow,Richie Rich,Ben Pol,Shaa,Master J
na baadhi ya walioshiriki kwenye Filamu hizo.Miongoni mwa filamu ambazo zimesambazwa na Proin Promotion mpaka sasa ni pamoja na ile ya Foolish Age aliyoigiza Lulu,Figo,Siri ya Mtungi,Long Time,Family Curse,Mapenzi ya Mungu na zingine kadhaa.



















































0 comments:
Post a Comment